Toleo Maalumu

Habari

ZANZIBAR YANG’ARA KIMATAIFA

Na MWANDISHI WETU RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa taasisi na wadau wa sekta ya utalii kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha Tanzania, ikiwemo Zanzibar, inaendelea kunufaika na tuzo na fursa za kimataifa katika sekta ya utalii.Rai hiyo imetolewa leo tarehe 12 Desemba 2025, Ikulu Zanzibar, baada […]

MWIGULU ACHARUKA

DodomaSELINA MATHEW NA FRED ALFRED WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, ameiagiza Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma, kubaini maeneo yenye mianya ya rushwa ambayo yamechangia baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kujilimbikizia mali kwa udanganyifu. Ameitaka sekretarieti hiyo kuanzisha kitengo cha taarifa za siri kuhusu mienendo isiyoeleweka ya watumishi wa umma, kisha uchunguzi […]

SERIKALI YAITA WADAU KUISAPOTI TAIFA STARS

Na AMINA KASHEBA SERIKALI imetoa wito kwa wadau wa soka na Watanzania kuisapoti timu ya Taifa Stars, kuhakikisha inafanya vizuri katika fainali za Kombe la Mataifa  Afrika (AFCON 2025), zitakazofanyikia nchini nchini Morocco. Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 21, mwaka huu hadi Januari 18, mwakani nchini humo ambapo Stars hivi sasa ipo Misri katika maandalizi […]

DK. SAMIA APOKEA HATI ZA MABALOZI, ATEUA VIGOGO PSSSF, TANESCO 

DODOMANA MWANDISHI WETU RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi watano walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao ambapo amesisitiza dhamira ya Tanzania kuimarisha ushirikiano unaojengwa kwa  misingi ya kuheshimiana, maendeleo ya pamoja na mahusiano mema. Katika halfa hiyo iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, Dk. Samia aliweka msisitizo kwamba Tanzania na serikali wanazotoka mabalozi hao, zinachangia dhamira ya pamoja katika kukuza biashara, uwekezaji na maendeleo. Pia, alisisitiza umuhimu […]

ONDOENI HOFU

>> Ni kauli ya Waziri Simbachawene, awataka wananchi kuendelea na maisha ya kawaida, serikali imejipanga kukabili tishio lolote >> Jeshi la Polisi lasema utulivu umetokana na operesheni za ushirikiano kati yao na vyombo vingine vya ulinzi na usalama Na ATHNATH MKIRAMWENI SERIKALI imesema hali ni shwari nchini, imewataka wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji mali […]

UCHAGUZI

WATANZANIA 37,647,235 KUPIGA KURA LEO

Na WAANDISHI WETU TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza maandalizi yote muhimu ya Uchaguzi Mkuu wa wa Rais, Wabunge na Madiwani, yamekamilika.Jumla ya wapigakura 37,647,235, wamethibitishwa kushiriki uchaguzi huo. Mwenyekiti wa INEC, Jaji Jacobs Mwambegele, amesema hayo kupitia taarifa ya tume hiyo na kusisitiza, uchaguzi huo, unafanyika kwa mujibu wa masharti ya Ibara […]

KISHINDO SIKU 60 ZA DK. SAMIA

Na MUSSA YUSUPH,Mwanza SHAMRASHAMRA za maandalizi ya mkutano wa kufunga kampeni za Uchaguzi Mkuu, zimeendelea kuutikisa Mkoa wa Mwanza ambapo Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuhutubia maelfu ya wananchi, wapenzi, wanachama na wakereketwa wa CCM. Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu, katika Uwanja wa CCM […]

DK. MWINYI AJAWA MATUMAINI KIBAO

Na HANIFA RAMADHANI, Zanzibar MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema wana matumaini kuwa CCM itashinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa kesho kutwa. Dk. Mwinyi alisema hayo, katika ufungaji kampeni za Uchaguzi Mkuu wa CCM, uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, Mjini Unguja Alisema kutokana na wingi wa wanachama […]

DK. NCHIMBI AELEZA MAFANIKIO YA KAMPENI ZA CCM NCHINI

Na NJUMAI NGOTA,UKEREWEMGOMBEA Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amefunga kampeni za Chama kwa kishindo huku akisema amezunguka takribani mikoa yote kwa mafanikio makubwa.Katika mikutano yake ya kampeni, Dk. Nchimbi, ameinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 na kumwombea kura za Urais, Dk. Samia Suluhu […]

MAAGIZO YA DK. MWINYI KWA WATUMISHI Z’BAR

Na MWANDISHI WETU, Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewasisitiza watumishi wa umma kuendelea kufanya kazi kwa uzalendo na uwajibikaji wakizingatia misingi ya utumishi na utawala bora ili kutoa huduma bora kwa wananchi. Amesema lengo la serikali ni kuimarisha zaidi maslahi ya watumishi wa umma nchini, kulingana na […]

Siasa

TULIENI NYUMBANI

>>Ni agizo la Waziri Mkuu Dk. Mwigulu >>Simbachawene  asema maandamano ni haramu Na IRENE MWASOMOLA SERIKALI imewataka wananchi wasiokuwa na ulazima wa kutoka leo, watulie nyumbani. Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, alipowasilisha salamu za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru, ambapo aliwatakia Watanzania kheri. Kupitia […]

KIHONGOSI ATOA MAAGIZO KWA MADIWANI 

Na ATHNATH MKIRAMWENI CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka madiwani kufanya kazi zinazobeba ajenda za wananchi, zitakazotoa majawabu ya kero katika maeneo yao. Pia, CCM imesema itaendelea kusimamia vyema misingi ya uadilifu kwa watendaji wa Chama. Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, jijini Dar es Salaam, alipozungumza na […]

WASIRA : VIJANA MSIKUBALI KUTUMIKA KUVURUGA AMANI

Na MWANDISHI WETU MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewataka vijana kutokubali kutumika kuvuruga amani na utulivu nchini kwa madai ya kudai haki. Amesema Tanzania haina uadui na nchi nyingine, lakini yapo baadhi ya mataifa, yanayoumizwa na kasi ya maendeleo iliyopo nchini. Amesema wanafahamu Tanzania inaelekea kujikomboa kiuchumi, hivyo kuondoka […]

TUTAILINDA NCHI YETU KWA GHARAMA – PM MWIGULU

Na ELIZABETH JOHN WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, ametoa wito kwa Watanzania, kuwa makini dhidi ya makundi ya watu wenye nia ovu ya kuichafua na kuiharibu Tanzania kwa maslahi binafsi. Dk. Mwigulu, amesema serikali itawalinda Watanzania na rasilimali zake zote kwa gharama yoyote kupitia vyombo vya ulinzi na usalama. Waziri Mkuu, aliyasema hayo kufuatia matukio […]

MAWAZIRI SABA NA MIKAKATI YA KAZI

Na WAANDISHI WETU, Dodoma ZIKIWA zimepita siku nane (Sawa na saa 192), tangu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan awaapishe mawaziri na naibu mawaziri, wametaja vipaumbele vyao katika utekelezaji wa majukumu yao vyenye dhamira ya kuwatumikia wananchi. Baadhi ya mawaziri baada ya kukabidhiwa vijiti vya kuongoza wizara zao, wameeleza walivyojipanga kutimiza ahadi zilizotolewa na Rais Dk. […]

Biashara

TASAF KIELELEZO CHA MAFANIKIO MIAKA 64 YA UHURU

NA SULEIMAN JONGO WATANZANIA wanaadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) ambao ulipatikana Desemba 9, mwaka 1961 huku kukiwa na mafanikio mbalimbali ya mfano. Kupatikana kwa Uhuru kunatokana na msukumo wa wananchi wa Tanzania Bara kutaka kujinasua katika makucha ya wakoloni ambayo hawakutoa nafasi kwa Waafrika weusi kujiletea maendeleo katika sekta mbalimbali zenye […]

SERIKALI YAIVALIA NJUGA TANZANITE

Na MWANDISHI WETU WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, amesema serikali imejipanga upya kuyatangaza na kuyainua madini ya Tanzanite kimataifa kupitia mkakati wa kurejesha hadhi ya jiwe hilo adimu duniani. Akizungumza katika mkutano na wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wa madini ya vito katika eneo tengefu la ukuta wa Magufuli, Mirerani mkoani Manyara, Waziri Mavunde, alisema hatua […]

DK. MWIGULU ATOA SIKU 10

Na MWANDISHI MAALUMU WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, ametoa siku 10 kwa watendaji wa taasisi zinazohusika na usafiri wa mwendokasi jijini Dar es Salaam, kuainisha maeneo ya kufanyiwa kazi haraka, kurejesha hali ya mpito wakati serikali ikitafuta suluhisho la kudumu. “Wizara ya Ujenzi, TANROADS, DART, UDART, OWM-TAMISEMI, TANESCO na wadau wengine, kaeni kuanzia leo (jana), […]

TRENI ZA JIJI DAR, DODOMA ZANUKIA

Na ELIZBAETH JOHN MAANDALIZI ya ujenzi wa njia za treni za mijini katika majiji ya Dar es Salaam na Dodoma yameanza rasmi, hatua inayotarajiwa kubadili kwa kiasi kikubwa mfumo wa usafiri wa abiria na kupunguza msongamano wa magari. Akizungumza Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni […]

SIMBASC YAITA MASHABIKI KWA MKAPA

Na NASRA KITANA WAKATI Simba ikitarajiwa kuvaana na Petro de Luanda kesho, uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi wamewaomba mashabiki wake kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuisapoti miamba hiyo. Simba itachuana na Petro de Luanda saa 10:00 jioni katika mchezo wa kwanza wa kundi D wa Ligi ya Mabingwa […]

Michezo

SERIKALI YAITA WADAU KUISAPOTI TAIFA STARS

Na AMINA KASHEBA SERIKALI imetoa wito kwa wadau wa soka na Watanzania kuisapoti timu ya Taifa Stars, kuhakikisha inafanya vizuri katika fainali za Kombe la Mataifa  Afrika (AFCON 2025), zitakazofanyikia nchini nchini Morocco. Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 21, mwaka huu hadi Januari 18, mwakani nchini humo ambapo Stars hivi sasa ipo Misri katika maandalizi […]

WANNE ‘BYE BYE’ YANGA

Na NASRA KITANA WAKATI dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufunguliwa rasmi, Januari 15, mwaka huu uongozi wa Klabu ya Yanga unatarajia kuwatoa kwa mkopo wachezaji wanne, kwenda kuongeza kiwango katika timu mbalimbali. Hata hivyo, taarifa za ndani zinaeleza kuwa timu hiyo imepanga kuwatoa kwa mkopo wachezaji wake wanne ambao ni Faridi Mussa, Denis Nkane, Aziz […]

BONDIA MWAKYEMBE KUTOA ZAWADI YA KRISMASI

Na AMINA KASHEBA BONDIA wa ngumi za kulipwa, Emmanuel Mwaykembe amehaidi kutoa zawadi ya sikukuu ya Krisimasi katika pambano lake la Punch To Punch’ litakalofanyika Jumapili ya wiki  hii. Mwakyembe atapanda ulingoni kuzichapa na Tionge Chingeni kutoka Malawi katika pambano lisilo la ubingwa raundi nane, uzito wa kati litakalofanyika Ukumbi wa The Sea View Dome […]

MASTAA YANGA, SIMBA WAPEWA PROGRAMU ZA MAZOEZI

Na NASRA KITANA WACHEZAJI wanaoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, wamepewa programu maalumu za mazoezi wanapokwenda nyumbani ili kulinda viwango vyao. Ligi Kuu Tanzania Bara, imesimama kwa muda kupisha michuano ya Fainali yza Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) 2025 inayotarajiwa kufanyika nchini Morocco. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema […]

MCHUJO MKALI  KOCHA SIMBA

Na NASRA KITANA BODI ya Wakurugenzi wa klabu ya  Simba,  imekaa kikao kizito kufanya mchujo wa maombi ya makocha zaidi ya 100 wanaotaka nafasi hiyo. Simba inasaka kocha mpya baada ya kumtema Dimitar Pantev aliyetambulishwa kama meneja akiitumikia kwa siku 61 baada ya kuwa na mwenendo mbaya ndani ya kikosi chao. Akizungumza na mwandishi wa […]

Mitandao ya Kijamii

Instagram

Tiktok

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?